HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 22 February 2017

Serikali haina mgogoro na filamu za nje kuuzwa hapa nchini – Waziri Nape

Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Nape Nnauye amesema serikali haina mgogoro na filamu za nje kuuzwa hapa nchini bali wasambambazaji wa nje na filamu za hapa nchi wanatakiwa kufuata utaratibu ambao serikali inautaka.

Waziri Nape ameyasema hayo alipokutana na wadau wa filamu ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wizara ya habari,utamaduni, sanaa na michezo kukutana na wadau wa wizara yake na sasa ni zamu ya wadau wa filamu kubwa kikubwa ni kuzungumzia sera ya filamu na kusikiliza maoni na malalamiko ya wadau wa filamu.
Alisema “Serikali hatuna mgogoro na filamu za kutoka nje, mgogoro wetu ni mmoja tu nikufuata utaratibu , ukifuata utaratibu hapa hata ukiuza mali za milioni 10 hakuna atakae kusumbua, fuata utaratibu, hatuwezi kuwabana watu wa filamu za ndani kufuata utaratibu halafu watu wa ndani wafanye wanavyotaka, haiwezekani. Nataka niwahakikishieni hakuna presha itakayo nibadilisha kwenye hilo kwasababu nasimamia sheria .”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad