HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 15 February 2017

PICHA: WANANDOA WALIOFUNGA NDOA YA SHILINGI 100 YA KENYA WAFUNGA NDOA TENA

Wanandoa nchini Kenya waliofunga ndoa iliyogharimu shilingi 100 tu ya Kenya, wamerejea kiapo chao cha ndoa yao jana katika Siku ya Wapendanao katika sherehe kubwa iliyoandaliwa na wasamaria wema. 
Habari za wanandoa hao zilisambaa kwenye mitandao ya jamii mwezi uliopita nchini Kenya na watu wengi walioguswa na tukio hilo waliamua kujitolea kuigharamia upya tena harusi yao hiyo ili iwe ya kumbukumbu.
Katika harusi ya kwanza wanandoa hao Wilson na Ann Mutura walifunga ndoa wakiwa wamevalia nguo za kawaida fulana na jinzi, na kuvishana pete za chuma kanisani. Harusi yao ya marejeo iliyofadhiliwa inakasiwa kugharimu dola 35,000.


Wanandoa Wilson na Ann Mutura wakifunga ndoa yao ya awali iliyogharimu kiasi cha sh 100 za Kenya sawa na sh 1,800 za Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad