HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 16 February 2017

NSSF YAKUTANA NA WAAJIRI WA MKOA WA DODOMA

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)  limeendesha semina maalum kwa waajiri wake wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu endelevu waliojipangia kukutana na waajiri wake ili kuendelea kuelezana umuhimu wa hifadhi ya jamii  kwa waajiriwa  wao  na pia kupata fursa ya kuambiana changamoto kutoka pande zote ili kushirikiana kuzitatua na kuboresha huduma kwa pande zote.

Akiwakaribisha waajiri hao katika semina hiyo, Meneja wa NSSF mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma aliwaambia waajiri hao kuwa huo ni urataribu endelevu waliojipangia wa kukutana nao na kuwataka watekeleze wajibu wao wa kuwaandikisha wanachama na kuleta michango kwa wakati ili kuwezesha Shirika kutoa mafao kwa wanachama wao kwa wakati na kwa usahihi na kuwakumbusha kuhusu sheria ya NSSF inayoruhusu kutoa adhabu kwa waajiri wanaposhindwa kuwasilisha michango kwa wakati.

Awali, Meneja Matekelezo wa Shirika hilo, James Oigo aliwaambia waajiri hao kuwa swala la hifadhi ya jamii ni muhimu kuliko ambavyo mtu anaweza kufikiri kwa kuwa kuna mfano wa wazee wengi ambao mnawajua wanaishi maisha duni  kutokana na kutokuwa katika mfumo wa hifadhi ya jamii.

NSSF imeendelea kuwa kinara katika mifuko ya hifadhi ya jamii katika wingi na ubora wa mafao na sasa imeelekeza nguvu zake katika uwekezaji wa viwanda kama fursa  ya kuendelea kuboresha mafao ya wanachama wake, kuongeza ajira na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Meneja Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), James Oigo akitoa Mada wakati wa Semina semina maalum kwa waajiri wake wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu endelevu waliojipangia wa kukutana na waajiri hao, iliyofanyika katika Ukumbi wa Veta, Mjini Dodoma.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma akizungumza wakati wa Semina semina maalum kwa waajiri wake wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu endelevu waliojipangia wa kukutana na waajiri hao, iliyofanyika katika Ukumbi wa Veta, Mjini Dodoma.
Kaimu Meneja Kiongozi wa Uhusiano na Masoko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salum Kimaro akitoa maelezo kwa wanasemina hao, iliyofanyika katika Ukumbi wa Veta, Mjini Dodoma.
Washiriki wa semina wakiajiandikisha.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Waajiri ambao ni wanachama ya NSSF, Mkoani Dodoma.
Meneja wa NSSF Dodoma, Rehema Chuma akibadilishana mawazo na Afisa masoko wa NSSF Amina Mbaga wakati wa semina ya waajiri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad