HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 1, 2017

NI VITA YA KIHISTORIA BURKINAFASO VS MISRI AFCON LEO.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Nusu fainali ya kwanza ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inayifanyika nchini Gabon inaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kuchezwa kati ya Burkina Faso dhidi ya Misri utakaochezwa kwneye dimba la Stade de l'Amitié, Libreville. Timu hizo zinakutana zikiwa zimetinga hatua hiyo baada ya kuziondoa timu za Moroco na Tunisia kwneye mchezo wa hatua ya robo fainali.


TAKWIMU 

Februari 25 1998, kwenye kombe la mataifa Afrika kwenye kombe ka Mataifa  Afrika timu zilikutana na Burkina Faso kufungwa kwa goli 2-0 dhid ya Misri.
Januari 01 2000, kwenye kombe la Mataifa Afrika zilikutana tena lakini Burkina Faso akiendelea kunyanywasa na Misri na kuambulia kipigo cha 4-2.
Februari 27 2016, zilikutana tena katika mchezo wa kirafiki na Misri kufanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-0.



BURKINA FASO



Hii ni mara ya kumi (10) kwa timu ya taifa ya Burkina Faso kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika, mara ya kwanza iliweza kushiriki michuano mwaka 1970.

Mwaka 1998 Burkina Faso ikiwa mwenyeji waliweza kushika nafasi ya nne na mafanikio makubwa iliyowahi kupata timu hii ni mwaka 2013 ambapo ilifika kwenye hatua ya fainali.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Burkina Faso ni Paulo Duarte, raia wa Ureno anayejulikana kwa jina la utani la  “Les Étalons” Ikiwa na maana ya Farasi.

Kikosi kamili cha Burkina Faso: 

Makipa: Herve Koffi (ASEC/CIV), Moussa Germain Sanou (Beauvais/FRA), Aboubacar Sawadogo (Kadiogo)

Mabeki: Ernest Congo (Khemisset/MAR), Yacouba Coulibaly (Bobo), Issoufou Dayo (Berkane/MAR), Bakary Kone (Malaga/ESP), Souleymane Kouanda (ASEC/CIV), Issoumaila Lengani (Happoel Ashkelon/ISR), Patrick Malo (Smouha/EGY), Issouf Paro (Santos/RSA), Steeve Yago (Toulouse/FRA)

Viungo: Cyrille Bayala (Sheriff Tiraspol/MDA), Adama Guira (Lens/FRA), Charles Kabore (Krasnodar/RUS, capt), Prejuce Nacoulma (Kayserispor/TUR), Bakary Sare (Moreirense/POR), Blati Toure (Omonia Nicosia/CYP), Abdoul Razack Traore (Karabuspor/TUR), Alain Traore (Kayserispor/TUR), Bertrand Traore (Ajax Amsterdam/NED), Jonathan Zongo (Almeiria/ESP)

Washambuliaji: Aristide Bance (ASEC/CIV), Banou Diawara (Smouha/EGY), Jonathan Pitroipa (Al Nasr/UAE.


MISRI

Haya yatakuwa mashindano ya 23 kwa timu ya taifa ya Misri inayifahamika kama Pharaohs, wanarejea katika michuano hii kwa mara ya kwanza baada ya kushiriki mara ya mwisho mwaka 2010.

Misri wanasalia  kuwa taifa bora, kuweka historia ya kushinda mataji mengi ya taji hili, mara 7 mwaka 1957,1959,1986,1998,2006,2008 na 2010.

Safari ya kwenda Gabon



Misri ilipangwa katika kundi moja na Nigeria na Tanzania katika michuano ya kufuzu kwa fainali ya mwaka huu. Kati ya mechi nne ilizocheza nyumbani na ugenini baada ya Chad kuondolewa katika michuano hiyo, ilishinda mechi tatu na kutoka sarena  hivyo kuongoza kundi la G kwa alama 10.

Hali ya kisiasa imekuwa ikielezwa kuwa moja ya sababu ya Misri kukosa kufika katika michuano hii tangu mwaka 2010, na kuwepo kwao huenda kukaleta ladha tofauti.

Kocha.
Kocha wa timu hii ni raia wa Argetina Héctor Cúper mwenye umri wa miaka 61, alianza kuifunisha Misri mwaka 2015 na ndio timu ya kwanza ya taifa kunolewa na Muargentina huyona  ambaye ana uzoefu mkubwa kufuza soka katika klabu mbalimbali.

Alianza kufundisha soka mwaka 1993, wakati huo akiifunza klabu ya Huracan na baadae  Internationale ya Italia kati ya mwaka 2001-2003, Mallorca 2004-2006 na Parma mwaka 2008. Kabla ya kupewa kibarua nchini Misri, alikuwa anaifunza Al Wasl FC kutoka Falme za Kiarabu kati ya mwaka 2013-2014.

Kikosi
Makipa: Ahmed El-Shennawy (Zamalek), Essam El-Hadary (Wadi Degla), Sherif Ekramy (Al Ahly) 

Mabeki: Ahmed Fathi (Al Ahly), Ahmed Elmohamady (Hull City – Uingereza), Mohamed Abdel-Shafy (Al-Ahli – Ksa), Karim Hafez (Lens – Ufaransa), Ahmed Hegazy (Al Ahly), Saad Samir (Al Ahly), Ahmed Dweidar (Zamalek), Ali Gabr (Zamalek), Omar Gaber (Basel – Uswizi).

Viungo wa Kati: Mohamed Elneny (Arsenal – Uingereza), Tarek Hamed (Zamalek), Ibrahim Salah (Zamalek), Abdallah El-Said (Al Ahly), Amr Warda (Panetolikos – Ugiriki), Ramadan Sobhi (Stoke City – Uingereza), Mahmoud Hassan ‘Trezeguet’ (Royal Mouscron – Ubelgiji). 

Washambuliaji: Ahmed Hassan ‘Koka’ (Braga – Ureno), Marwan Mohsen (Al Ahly), Mahmoud Abdel-Moneim ‘Kahraba’ (Al-Ittihad – Ksa), Mohamed Salah (As Roma – Italia).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad