HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 3 February 2017

MATUKIO KATIKA PICHA: YANGA YANDELEA KUJITANUA KILELENI MWA LIGI KUU, YAIPA KICHAPO STAND UNITED CHA BAO 4-0

 Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bars, Yanga wameendelea kukaa kileleni baada ya kutoka na ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Stand United ya Shinyanga kwenye mchezo uliochezwa leo katika dimba la uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ambao ulianza kwa kasi na katika dakika ya 17 Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma anaipatia timu yake bao la kwanza na la kuongoza akiunganisha krosi safi ya Simon Msuva, ambapo dakika ya 26, Yanga wanaandika goli la pili kupitia kwa mshambuliaji wake wa pembeni, SimonMsuva.

Mpaka mapumziko Yanga wanatoka wakiwa wanaongoza kwa goli mbili, dakika 45 za kipindi cha pili inaanza Obrey Chirwa anaipatia Yanga goli la tatu.

Nahodha Nadir Haroub 'canavaro' katika dakika ya 79 anaipatia Yanga bao la nne na la ushindi akiunganisha kona safi iliyopigwa na Juma Abdul na mpaka filimbi ya mwisho inamalizika Yanga wanatoka kifua mbele kwa goli 4-0.

Baada ya matokeo hayo, Yanga wanakwea kileleni kwa alama 49 akifuatiwa na Simba mwenye alama 45 ambaye kesho anacheza na Majimaji.
 Kikosi cha Yanga.
 Kikosi cha Stand United.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad