HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 11 February 2017

SIMBA YAONGOZA LIGI KWA MARA NYINGINE,YAIFUNGA PRISONS BAO 3-0

Timu ya Simba imejikita kileleni baada ya kutoka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya maafande wa Tanzania Prison  kwenye mchezo uliochezwa leo katika dimba la Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ulioanza kwa kasi kila timu ikitafuta goli la kuongoza, ilichukua dakika 18 kwa Simba kupata goli la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake Juma Luizio.

Katila dakika ya 28, Ibrahim Ajib anaipatia Simba goli la pili akipokea pasi safi ya Laudit Mavugo na mpaka kufika mapumziko Simba 2-0.


Kipindi cha pili kilianza kwa Prison kutafuta goli kwa kila namna lakini Laudit Mavugo anaipatia Simba goli la tatu na la ushindi katila dakika ya 57.

Mpaka mpira unamalizika Simba wanatoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 3-0 na kufikisha alama 51 akifuatiwa na Yanga wenye alama 49.
 Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Laudit Mavugo akijaribu kuupiga mpira kwa mtindo wa Tik Tak mbele ya Mabeki wa Timu ya Tanzania Prisons, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliochezwa katika uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam jioni ya leo. Simba imeshinda bao 3-0.
 Mshambuliaji wa Timu ya Tanzania Prisons, Benjamin Asukile akichuana vikali na James Kotei wa Simba, Beki Mohamed Hussein "Tshabalala" akingalia namna ya kusaidia wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda bao 3-0.
 "Huondoki na mpira hapa"

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad