HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 28 February 2017

KIWANDA CHA VIGAE CHALINZE KUAJIRI WATU 6000

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KIWANDA cha Vigae cha Twayfod kinatarajia kuajiri watu 4000 wa moja kwa moja na pamoja na ajira za muda mfupi 2000.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji  nchini, Clifford Tandari amesema kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya Tanzania ya viwanda imeanza kutimia.
Tandari amesema kuwa wanaendelea kuchakata makampuni mbalimbali ambayo yameonyesha dhamira ya kutaka kuwekeza katika sekta ya viwanda hivyo ni fursa ya watanzania kuchangamkia ajira zinazojitokeza.
Ameongeza kuwa kiwanda cha vigae kitakachojengwa katika mji wa Chalinze kitatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ambapo kuna maeneo yatapata mapato yatayotokana na malighafi hizo.
Ameongeza kuwa kiwanda cha vigae kitaanza hivi karibuni hivyo watu wakae tayari kuchangamkia fursa za awali ajira zitakazotolewa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TIC), Clifford Tandari akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ya uwekezaji wa viwanda uliofikiwa katika nchi naja  jijini Dar es Salaam. picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad