HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 21 February 2017

JESHI LA POLISI LAMUACHIA MWENYEKITI WA CHADEMA BAADA YA KUMSHILIKIA KWA TAKRIBANI MASAA 10

Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalim inaeleza kuwa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, limemuachia Mwenyekiti wa Chama hicho na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe usiku wa kuamkia leo baada ya kumshikilia kwa takribani masaa 10 kwa mahojiano juu ya tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevywa. 

Mbowe alikuwa ni mmoja katika orodha ya majina 65 ya wanaodaiwa kuwa vinara wa biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya hapa nchini iliyotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad