HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 4 February 2017

Fedha ya umma inatakiwa kuheshimiwa - kaimu mkurugenzi mtendaji PSPTB


Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi, akizungumza kabla ya kumkaribisha kaimu mkurugenzi mtendaji wa PSPTB, 
Godfred Mbayi  (katikati) kuzungumza washirikiwa warsha hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya taaluma PSPTB, Ally Songoro.

Na Chalila Kibuda.

Fedha ya umma inatakiwa kuheshimiwa kutokana na majukumu yake ya kuhudumia wananchi.

Hayo yalisemwa na kaimu mkurugenzi mtendaji wa bodi ya manunuzi na ugavi (PSPTB), Godfred Mbayi wakati wa kufunga mafunzo ya masuala ya manunuzi katika taasisi ya moyo ya jakaya kikwete (JKCI), amesema fedha ya umma ikiheshimiwa maendeleo yatapatikana tu.

Mbayi amesema kuna nchi zilianza na Tanzania zimeweza kufika mbali katika matumizi ya fedha za umma. Amesema kazi ya manunuzi inatakiwa kufanyika kwa mfumo wa pamoja kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

Ameongeza kuwa ili manunuzi yafanyike, maadili ya wataalam yanahitajika kwa kuangalia uzalendo kwanza wa nchi. Hata hivyo amesema kuwa hakuna ugumu katika kufanya manunuzi  kinachohitajika ni kufuata sheria.
 Mwanasheria kutoka taasisi ya PPAA , Hamis Tika akizungumza na watumishi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.
Baadhi ya wafanyakazi wa tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakisikiliza kwa makini juu ya mafunzo ya masuala ya manunuzi.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya taaluma PSPTB, Ally Songoro akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete .

Afisa Mwanadamizi wa Mahusiano ya Umma na Masoko Shamim Mdee na mratibu mkuu wa utafiti na ushauri PSPTB Amos Kazinza wakifuatilia mafunzo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad