HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, February 5, 2017

DIWANI DEBORA SANGA AZINDUA KAMPENI YA ‘TUNAWEZA’ WILAYA YA ILALA ILIYO CHINI YA KITUO CHA MSAADA WA SHERIA WLAC.

Na Karama Kenyunko, Globus ya JamiiForums.

Watanzania wameaswa kuacha Tabia ya kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa baadhi ya wanawake na watoto. 

Hayo yalisemwa na Diwani wa viti maalum (Chadema), Kata ya Segerea, Deborah Sanga Kwenye mkutano wa kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika kwenye shule ya msingi Tabata jijini Dar es Salaam. 

Alisema ikiwa wananchi watabaini vitendo hivyo wanapaswa kutoa taarifa mara moja katika mamlaka husika pindi wanapogundua kuwepo kwa ukatili huo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria. 

Naye Kaimu Mkurugenzi wa WLAC Wigayi Kissandu, amesema kuwa ukatili huu unamadhara makubwa sana hasa kwa wanawake na watoto. Alisema kuwa vitendo vya ukatili huu wa kijinsia vmejikita zaidi katika mila na desturi na sheria mbali mbali zinazotumika ambazo ni kandamizi. 

" Ili kupunguza au kumaliza kabisa ukatili huu inapaswa kutungwa sheria mpya zitakazomaliza sheria kandamizaji dhidi ya mwanamke kama zile za mirathi na ndoa ili kuweza kumkomboa mwanamke," alisema. 

Aidha aliongeza kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vipo kwa kiasi kikubwa na kwamba katika kipindi cha Januari mwaka huu WLAC kimeshapokea kesi 150 mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia. 

Kwa upande wake Inspekta Stella Mindasi wa Dawati la Jinsia la watoto kituo cha polisi Tabata, alisema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja, januari hadi Desemba 2016 jumla ya kesi 165 zimelipotiwa zikiwemo kubaka 24 , kulawiti 15 shambulio la kimwili 37 shambulio la aibu 6 shambulio 51, kutoa luhha yabmatusi 8 kijeruhi 15, kitelekeza familia 7, kutorosha mwanafunzi. 

Katika matukio hayo jumla ya kesi 30 zimekwishashatolewa hukumu.
Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kulia) akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa na Mwanasheria WLAC, Wigayi Kisandu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. Picha na Muhidin Sufiani Mafoto Blog
Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya vitabu Consoler Eliya kutoka New Hope for Girls Orphan, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kushoto) akiwakabidhi zawadi ya vitabu Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zawadi, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
Mgeni rasmi Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga, akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. 
Wasanii wa Kikundi cha Msimamo Sanaa Group,wakiigiza mbele ya mgeni rasmi na wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. 

Consoler Eliya kutoka New Hope for Girls Orphan, akizungumza wakati akitoa ushuhuda wa Vitendo vya Unyanyasaji kwa Wanawake alivyowahi kuvipitia. Consoler alikuwa kitoa ushuhuda huo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi huo wakiwa meza kuu.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule mbalimbali za Sekondari waliojitokeza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.

Wasanii wa Kikundi cha Msimamo Sanaa Group,washambulia jukwaa wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad