HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 5 February 2017

BEN POL AACHIA VIDEO YA 'PHONE'


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol, ameachia video ya wimbo wake mpya unaitwa 'Phone' aliyomshirikisha mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Mr. Eazi. Akizungumza na Globu hii, Pol alisema kuwa wimbo huo ameutengeneza katika studio ya One love records, iliyopo jijini Dar es Salaam chini ya mtayarishaji Tiddy Hotter. 

Alisema tayari wimbo huo upo mtaani kwa video yake kuonekana ikiwa imetangulizwa na wimbo ambao ulitoka kwa audio. 

Aidha Pol amewataka wapenzi wa muziki nchini waanalie ujio wa video hiyo ambao ana amini kila atakayepata nafasi ya kuiona. 

"Nashukuru nimemaliza kurekodi na tayari video nimaenza kusambaza katika vituo mbalimbali vya Televisheni na katika mitandao mbalimbali, nina amini kila mdau anaipenda na kukubali ujio wa Phone. 

Pol alisema ujio wa wimbo huo ni moja ya mipango yake ya mwaka 2017 na ameanza kwa kutoa wimbo huo wa 'Phone'. 

"Wimbo wa Phone ni moja ya malengo yangu ya mwaka huu na ndiyo ujio wangu wa 2017, naomba wapenzi waupokee na kuusikiliza kila mtu ataelewa nini nimejipanga kupitia mwaka huu"alisema Pol. 

Mwanamuziki huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo pamoja na, Moyo Mashine, Maneno, Sofia, Pete, Maumivu, Samboira na ameshirikishwa kwenye wimbo wa Darasa unaotamba kwa sasa nchini unaitwa muziki. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad