HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 22 February 2017

AGNES GERALD "MASOGANGE" APANDISHWA MAHAKAMANI LEO

Mrembo anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald Way maarufu kama Masogange au Deal (28), amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kutumia dawa za kulevya.
Mrembo huyo anayeishi Makongo Juu ambaye alikuwa akitumia muda mwingi kujiziba sura yake kwa mtandio na miwani ya Giza alisomewa tuhuma zake mbele ya Hakimu Mkazi Willbard Mashauri. Hata hivyo, ameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama.
Mahakama ilimtaka Masogange kuwekwa dhamana ya milioni kumi hali kadhalika na wadhamini wake wawili nao walitakiwa kuwekwa kiasi hicho cha fedha.
Aidha mahakama imemuamuru kutosafiri nje ya Dar ea Salaam bila ya kupata kibali cha Mahakama.
Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali, Constantine Kakula amedai kuwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu katika Eneo na Wilaya isiyojulikana lakini ndani ya jiji la Dar es salaam, Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).
Katika hatua ya pili, Mshtakiwa Masogange siku na mahali pasipojulikana alitumia dawa za kulevya aina ya OXazempam.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Masogange amekana kujihusisha na tuhuma hizo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21, mwaka huu.
 Mrembo anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald Way maarufu kama Masogange au Deal (28) akielekea kwenye chumba cha Mahakama ya  Hakimu Mkazi  Kisutu ambapo alisomewa Mashtaka ya Matumizi ya Dawa za Kulevya.
  Mrembo anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald Way maarufu kama Masogange au Deal (28)akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kutimiza masharti ya dhamana leo jijini Dar es Salaam.
Agnes Masogange akitoka katika Mahakama hiyo akiwa na Wakili wake, Nictagon Itege baada ya kutimiza masharti ya dhamana leo ijini Dar es Salaam.
 Agnes Masogange akiondoka katika Mahakamani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad