HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 29, 2017

WACHEZAJI WANAWAKE WAJIPANGA MIAKA 10 YA LUGALO GOLF CLUB

Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ

IDADI  ya Wanawake wanaojiandaa  na mashindano ya miaka 10 ya klabu ya golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania  imeongezeka na kuongeza joto la maadhimisho ya klabu hiyo yanayotarajiwa kufanyika mwezi Februari Jijini Dar es salaam.

Mmoja wa wachezaji hao ni aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Wanawake Hawa Wanyenche ambaye kwa muda mrefu hakuwa akionekana viwanjani kucheza lakini sasa ameibukia katika klabu ya Lugalo.
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake Hawa Wanyenche akiwa katika mazoezi kujiandaa na mashindano ya maadhimisho ya miaka 10 ya klabu ya gofu ya JWTZ yanayotarajiwa kufanyika februari jijini Dar es salaam.


Akizungumza wakati wa mazoezi yake katika klabu ya lugalo Hawa alisema anaona kiwango chake kinaanza kurejea kutokana na kutokuwa uwanjani muda mrefu na anaamini kuibuka na ushindi katika mashindano hayo na yeyote yajayo ili kurejesha heshima yake.

“ Unajua ni muda mrefu sijaingia uwanjani na falsafa yangu ni kuishinda sio kushindwa na siri ya kushinda ni mazoezi ndio maana nimeanza mapema hivyo wanawake wengine wanajua wako vizuri katika golf waje tupambane”. Alisema Hawa.
Aliongeza kuwa ni wakati muafaka kwa Wachezaji wengine wa Vilabu vingine nao kujipanga na kuhakikisha wanashiriki ili kufanikisha mashindano lakini pia kuzihirisha uwezo wao.
Mchezaji Nicholous Chitanda (katikati) wa klabu ya Lugalo akiwa katika mazoezi kujiandaa na mashindano ya maadhimisho ya miaka 10 ya klabu ya gofu ya JWTZ yanayotarajiwa kufanyika februari jijini Dar es salaam.

Naye Mchezaji Vicky Elias alisema  muda umekwisha na ukizingatia kuna uwezekano wa wachezaji  kutoka katika nchi mbalimbali kuja kushiriki michuano hiyo hivyo mazoezi pekee ndio yatakayowafanya kuibuka na Ushindi.
“ Wachezaji wengi wamekamia mashindano haya lakin I nitashinda ingawa nikishindwa nitakubaliana kwa kuwa ni moja ya matokeo katika Golf kwani mchezo huo hautabiriki” Alisema Vicky.

Kwa Upande wake mchezaji Chipukizi Habiba Likuli alisema  kikubwa ni kukabiliana na ushindani na kuibuka na ushindi na kulibakiza kombe la historia kwa klabu.
Mchezaji Habiba Likuli wa klabu ya Lugalo akiwa katika mazoezi kujiandaa na mashindano ya maadhimisho ya miaka 10 ya klabu ya gofu ya JWTZ yanayotarajiwa kufanyika februari jijini Dar es salaam.


“ Mashindano yaliyopita nilicheza katika kundi la Watoto Junior lakini kutokana naKiwango changu ninaimani nitakuwa na uwezo wa kuchezea kundi la Wanawake Ladies katika mashindano hayo kama kanuni zitaruhusu” Alisema Habiba.
 Kwa upande wake  Kapteni wa Klabu ya golf ya Lugalo Kapteni Japhet Masai alisema  katika kuyapa uzito mashindano hayo  wamepeleka mialiko katika nchi za Zambia,Kenya,Malawi ,Zimbambwe , Rwanda na Uganda.

Aliongeza kuwa tarehe na mgeni Rasmi katika Mashindano hayo anatarajiwa kutangazwa na mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Jumanne saa nne katika Klabu hiyo.
Mchezaji wa klabu ya lugalo Vicky Elias ( wakwanza kushoto) akipiga mpira wakati wa mazoezi kujiandaa na maadhimisho ya miaka 10 ya klabu hiyo jijini Dar es salaam. wanaomtazama ni Hawa Wanyenche (katikati) na Salim Mwenyenza (kulia). (picha na Luteni Selemani Semunyu).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad