HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 19, 2017

WAAMUZI WAMETUNYIMA USHINDI DHID YA MBEYA CITY- AZAM


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Baada ya kulazimishwa sare na Mbeya City katika mchezo wa jana uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi, benchi la ufundi la Azam umelalamikia maamuzi mabovy ya waamuzi waliochezesha mechi hiyo.



Wakitoa malalamiko hayo kupitia mtandao wao, wamelalamikia maamuzi yaliyokuwa yakifanywa na waamuzi hao katika dakika 45 za kipindi cha pili na kushangaza watu wengi hadi wachezaji uwanjani na kusema kuwa wanaamini kuwa hayo yalikuwa  yakifanywa na waamuzi kana kwamba wakitaka mtanange huo uishe kwa sare.


Kwenye mechi hiyo  mwamuzi wa kati alikuwa ni  Florentina Zabron akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Josephat Bulali na namba mbili, Gasper Ketto.

Malalamiko hayo yanakuja zaidi hasa baada ya mwamuzi Florentina, kushindwa kufanya maamuzi tukio la kufanyiwa madhambi ya makusudi mshambuliaji wa Azam FC, Shaaban Idd na beki Haruna Shamte wakati akimiliki mpira ndani ya eneo la hatari kuelekea langoni mwa Mbeya City.

Licha ya dakika nyingi kupotezwa kwa mbinu za upotezaji muda za wachezaji wa Mbeya City katika vipindi vyote, mwamuzi wa akiba Omary Kambangwa alionyesha dakika nne tu za nyongeza.

Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 31 na kubakia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, ikizidiwa pointi 14 na kinara Simba mwenye pointi 45, ambayo nayo imelazimishwa suluhu na Mtibwa Sugar jana.

Katika mchezo huo Azam FC imewekuwa timu ya kwanza kuanza  kutumia ubao wa kielektroniki wa kubadilishia wachezaji.

Kikosi cha Azam FC leo:

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Himid Mao/Domayo dk 59, Salum Abubakar, John Bocco (C), Yahaya Mohammed/Afful dk 74, Joseph Mahundi/Shaaban

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad