HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 13, 2017

UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE WANUSURIKA KUWAKA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), usiku wa kuamkia leo umenusurika kuteketa kwa moto uliozuka ghafla na kusababisha taharuki kwa wasafiri na watumiaji wa uwanja huo, hali iliyolazimu kusimamishwa kwa shughuli zote uwanjani hapo.

Vikosi vya Zimamoto vilifika eneo la tukio kwa wakati na kuanza kukabiliana na moto huo ambao walifanikiwa kuuzima.

Akizungumza baada ya tukio hiho, Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Kamishna Msaidizi (SACP), Martin Otieno amesema kuwa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo na kwamba uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha moto huo na hasara iliyosababisha, unaendelea kufanyika na kwamba tayari shughuli zote za uwanjani hapo zimerejea na zinaendelea kama kawaida.

Aidha Meneja wa Uwanja huo amewatoa hofu Watanzania na wasafiri wote wanaotumia Uwanja huo, kwa kuwaeleza kuwa hali imekuwa shwari uwanjani hapo na huku akikiri  kutokea kwa moto huo unaodaiwakuwa ulizuka kuanzia majira ya saa 6 hadi saa 7 usiku wa kuamkia leo.

Ambapo ameeleza kuwa shughuli zote za usafirishaji zimehamishiwa uwanja wa zamani (Terminal One) na kule zinaendelea kama kawaida huku wakiweka sawa maeneo yalioathirika na moto. 


“Madhara kidogo yametokea kwenye jengo la kuhifadhia mizigo pekee, hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa kutokana na moto, mashine zote zipo salama na sasa shughuli zote za usafirishaji tumezihamishia kule uwanja wa zamani (Terminal One) zinaendelea kama kawaida”. Amesema Meneja huyo.
Kwa mbali kule ni sehemu ya moto huo ulipoekuwa ukiendelea kuwaka.
Giza lilitawala katika eneo lote la jengo la Uwanja wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad