HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 31, 2017

TAASISI MPYA YA KILIMO YAZINDULIWA NCHINI, NI AGRO FOR HELP

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandiliwa akikata utepe kuzindua taasisi mpya ya kilimo ya Agro for help, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PSPF, Jijini Dar es salaam. kushoto ni wakurugenzi wenza wa taasisi hiyo Neema Shukuru na Mwaka Mohamed.

Na Humphrey Shao, Globu ya jamii.

Wito umetolewa kwa wananchi mbalimbali kujikita katika kilimo ili kuendana na mabadiliko ya uchumi hapa nchini kuelekea katika uchumi wa Viwanda.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandiliwa wakati wa ufunguzi wa taasisi isiyo ya kiserikali inayohusu kilimo ya Agro for Help Foundation.

“katika kuelekea uchumi wa viwanda ni lazima tuwe na kilimo cha uhakika kwani watu wengi sana wamekuwa wakilima pasipokuwa na elimu ya kutosha hivyo kufanya kilimo kisichokuwa na tija” amesema Mgandilwa.

Kwa upande wake muwasisi wa taasisi hiyo, Mwaka Mohamed amesema kuwa wameamua kuanzisha taasisi hiyo ili kuweza kuwasaidia wakulima ambao wengi wao hawana elimu sahihi juu ya kilimo chenye tija.

Amesema kuwa Agro for help Foundation ipo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mkulima wa Tanzania anapata msaada wa kutosha wa mtaji, pembejeo na namna gani wanaweza kufanya kilimo cha kisasa kwa kuunganishwa na wadau mbalimbali wa kilimo.

Aidha ametoa wito kwa wadau wote wenye malengo ya kuhakikisha kuwa kilimo cha Tanzania kinakuwa kwa kuweza kushirikiana na Agro for help Foundation kwa maslahi ya wakulima.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandiliwa akizungumza na wadau wa kilimo wakati wa uzinduzi wa taasisi mpya ya kilimo ya Agro for help, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PSPF, Jijini Dar es salaam. 
Henry Kazula kutoka Jielimishe akizungumza na wadau mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa taasisi mpya ya kilimo ya Agro for help, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PSPF, Jijini Dar es salaam. 
baadhi ya wadau waliofika katika mkutano huo wakifatilia kinachoendelea
waasisi wa taasisi mpya ya kilimo ya Agro for help, Neema Shukuru na Mwaka Mohamed wakimkabidhi ripoti mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad