HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 23, 2017

RC MAKALLA ATEMBEA VITUO VIWILI VYA REDIO JIJINI MBEYA LEO, AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MKOA HUO MOJA KWA MOJA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla leo Januari 23, 2017 amefanya ziara ya kutembelea vituo viwili vya Redio vilivyopo mkoani humo, na kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na wananchi wa Mkoa Mbeya.

Makalla alisema ameamua kutembelea vituo hivyo ambavyo vimemuwezesha kuzungumza na wananchi moja kwa moja ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao, Makala alivichaguwa vituo hivyo kwa kuwa ndivyo kituo pekee kufanya mahojiano ya moja kwa moja na wananchi wa mkoa wa Mbeya tangu aingie rasmi mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza moja kwa moja na wananchi wa Mkoa wa Mbeya, kupitia kituo cha Redio 91.3 Dream FM cha mkoani humo, ikiwa ni sehemu yake ya ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari vilivyomo kwenye Mkoa huo.Picha na Fadhiri Atick Mmg Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akisaini kitabu cha wageni wakati alipofika kukitembelea kituo cha Redio 91.3 Dream FM cha mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akipokea kitabu cha usimamizi wa biashara na fedha kilicho andaliwa na Fred Matola Msemwa, kutoka kwa Meneja masoko wa Redio 91.3 Dream Fm ya jijini Mbeya, Sam Mhina.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiangalia moja vya vifaa vya kurushia matangazo wakati alipotembelea Kituo cha Redio 106.5 Big Star Fm cha jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akifanyiwa mahojiano ya moja kwa moja na Mtangazaji wa Kituo cha Redio 106.5 Big Star Fm cha jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Redio 106.5 Big Star Fm cha jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza jambo na Mkurugenzi wa kituo cha redio Big Star Fm 106.5 Mbeya, Kura Mayuma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad