HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 24, 2017

RAIS DK.JOHN POMBE MAGUFULI KUZINDUA MRADI WA UDART KESHO JIJINI DAR ES SALAAM.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Rais Dk. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (UDART) katika kituo cha mabasi Gerezani –Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa kampuni ya mabasi yaendayo Haraka (UDART), Deus Buganywa amesema katika uzinduzi barabara ya Msimbazi itafungwa na mabasi yatakwenda kugeuzia katika kituo cha Feri.

Amesema safari za mabasi zitasitishwa mpaka pale uzinduzi utakapo kuwa umekwisha na kurejea katika hali ya kawaida.

Buganywa amesema kwa abiria wanatumia kituo cha Gerezani watashuka katika kituo cha zimamoto ‘Fire’ na mabasi hayo yataendelea mpaka kituo cha Feri.

Kampuni ya mabasi hayo inawaomba radhi abaria wanaoshuka katika vituo vya msimbazi hadi Gerezani kwa usumbufu ulioitokeza.
Afisa Habari wa kampuni ya mabasi yaendayo Haraka (UDART), Deus Buganywa akizungumza na waandishi habari juu ya uzinduzi mradi wa mabasi yaendayo haraka kesho jijini Dar es Dar es Salaam.
Sehemu waadishi wa habari wakimsikiliza Afisa Habari wa kampuni ya mabasi yaendayo Haraka (UDART), Deus Buganywa, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jami.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad