HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 24, 2017

MOUNT MERU RICKERNEST MUSIC BAND YAJA KWA KASI JIJINI ARUSHA

Bendi mpya ya mziki wa dansi ijulikanayo kwa jina la Mount Meru Ricknest imezinduliwa rasmi mkoani Arusha huku ikiwaahidi wapenzi wa muziki wa dansi burudani isiyokuwa na mpinzani.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, mmoja wa wakurugenzi wa bendi hiyo, Ernest Mlolere alisema kuwa kwa sasa wameitambulisha bendi hiyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na wanataajia kuizindua rasmi rasmi katika siku yawapendanao (valentine day ) hapa hapa jijini Arusha

Alibainisha kuwa bendi hiyo ipo chini ya wakurugenzi watatu akiwemo yeye mwenyewe Erinest Mlolere, Denis Kaiza pamoja na Prisca Aloyce ambapo wamekaa chini na wakaamua kuanzisha bendi hiyo ili kuweza kuwapa burudani wakazi wa mkoa wa Arusha, ambao wamekuwa wakikosa burudani ya bendi ya uhakika kwa kipindi cha muda mrefu

Aidha aliongeza kuwa bendi hii haitakaa Arusha tu bali itakuwa inatembea mikoa mbalimbali ili kuweza kuwapa burudani wapenzi wa muziki wa dansi wa nchi nzima .

Alibainisha kuwa katika bendi hiyo pia kuna wana muziki kutoka katika bendi maarufu za nje ambapo alitaja baadhi ya wanamuziki waliotoka katika bendi za nje kuwa ni pamoja na rais wa bendi Fabrice Kinyenya (kulialia) ambapo yeye ametoka katika bendi ya Ferre Gola pamoja na Katoto (Tanesco) ambaye yeye ametoka katika bendi ya Fally Ipupa wote .

Hii ni bendi ya tatu kuzinduliwa ndani ya jiji la Arusha kwani kipindi cha mwaka uliopita 2016 bendi mbili zilianzishwa jijini hapa ambapo bendi ya kwanza ya Mjengoni ilizinduliwa na pia kuna bendi ya East Afrika, hivyo wakazi wa jiji hili wamenufaika kwa kuletewa muziki karibu tofauti na kipindi cha nyuma ambapo wakazi wa jiji hili walikuwa wakipata tabu sana kupata burudani ya muziki wa live bandi .
Rais wa bendi ya Mounti Meru Rickernest, Fabrice Kinyenya "kulialia" akiimba katika usiku wa kuitambulisha bendi hiyo kwa wakazi wa jiji la Arusha
wanamuziki wa bendi ya Mounti Meru Rickernest wakionyesha kiwango chao ndani ya ukumbi wa Triple A jijini Arusha
waimbaji wa bendi ya Mounti Meru Rickernest wakifanya yao

Wanenguaji wa bendi ya Mount meru Rickernest wakifanya yao.

Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad