HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 31, 2017

MKWASA RASMI YANGA, APEWA UKATIBU MKUU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


UONGOZI wa klabu ya Yanga umemtangaza aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo na mchezaji wa zamani wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Vodacom Charles Boniface Mkwasa kuwa katibu mkuu akichukua nafasi ya Baraka Deusdedit anayerejea kwenye Idara yake ya Fedha.

Kocha huyo ambaye pia amewahi kuifundisha Yanga ameingia kandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia Yanga. 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kwamba Mkwasa anaanza majukumu yake rasmi Februari 1, mwaka huu na sababu kubwa ya kumchagua Mkwasa ni kuimarisha safu ya uongozi wa klabu hiyo ambapo aliyekuwa kaimu katibu mkuu, Baraka Deusdedit anarejea katika nafasi yake ya zamani ya Ukurugenzi wa Fedha.

Sanga alisema kuwa wanajua kuwa Mkwasa ana uwezo mkubwa wa kuitumukia vema nafasi hiyo na kuleta maendeleo na mabadiliko ndani ya Yanga na nafahamu watu watashangaa na kujiuliza sababu ya kupatiwa nyadhifa hiyo ila kiukweli ana uzoefu mkubwa katika kazi hiyo tofauti na watu wanavyomuelewa.

“Na hii si mara ya kwanza, hata Zambia, Kalusha Bwalya amewahi kuwa katibu mkuu wa chama cha soka nchini humu huku wakijua kuwa ni mchezaji mstaafu au kocha, Yanga tumemuona Mkwasa ni bora ya zaidi katika nafasi hiyo,” alisema Sanga.

Kwa upande wake Mkwasa alisema kuwa nafasi hiyo aliyopewa ni kubwa na nyeti sana katika masuala la soka sehemu yoyote. Alisema kuwa kwa sasa yupo tayari kujitolea kadri ya uwezo wake kuhakikisha Yanga inakuwa na kufikia malengo yake kwa wakati uliopongwa.

Mkwasa alisema kuwa mbali na kuitumikia nafasi hiyo mpya atakuwa tayari kushirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo kwa maslahi mapana zaidi ya timu. "Kwa sasa napenda kuwaahidi wanayanga wote kuwa nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha tunailetea klabu yetu maendeleo na nitahakikisha tunafanya vizuri ndani na nje ya nchi", alisema Mkwasa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad