HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 30, 2017

MBUNGE VITI MAALUM IRINGA ROSE TWEVE AFANYA ZIARA KATIKA KATA MBILI ZA MKOA HUO

Na Ripota wa Globu, Iringa


Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve ameanza rasmi kutimiza ahadi zake za kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuangalia namna ya kuwasaidia wakina mama wa mkoa huo kujiinua kiuchumi.

Katika ziara hiyo mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Rose ameanza kutimiza ahadi zake alizowaahidi wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 ndani ya jumuiya ya UWT mkoa wa Iringa.

Ziara yake ya kwanza imeanza Januari 28 2017 katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa na kutembelea kata za Mtitu na Ukumbi na aliweza kuongozana na mbunge viti maalumu kutoka mkoa wa Songwe Juliana Shonzana pamoja na viongozi wa UWT wilaya ya Kilolo.

Pamoja na mambo mengine Rose ametoa jumla ya shilingi za kitanzania milioni moja na laki tisa ( 1,900,000) kwa jumuiya ya akina mama (UWT) wilaya ya Kilolo kwa ajili ya kujiimarisha na kuinua vikundi vya vya akina mama wa jumuiya hiyo. 

Rose anaamini kuwa UWT ni kiungo kikubwa na muhimu ndani ya Chama cha Mapinduzi hivyo kama jumuiya ikiwa imara kwa kupitia miradi mbali mbali basi italeta hamasa ndani ya chama na ameahidi kuwa ziara hii ni endelevu na itakuwa ya mkoa mzima.
Mtendaji Agentina Myovela (kulia) na diwani wa viti maalum wa kata ya ukumbi wilaya ya kilolo Rehema Nyasi wakitoa maelezo kwa Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve (katikati) juu ya ujenzi wa kituo cha afya kinachoendelea kujengwa katika kata hiyo.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve akipata maelezo kutoka Kwa katibu wa UWT Wilaya Yusuph Mgovole juu ya ujenzi wa ukumbi wa jumuiya hiyo ambapo aliweza kuchangia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) Kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve (wa pili kulia) akikabidhi kiasi cha pesa shilingi laki Saba (700000) kwa akina mama wa UWT kata ya Mtitu katika ziara aliyoifanya mwishoni mwa wiki ikiwa ni moja ya ahadi zake za kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuwainua akina mama wa mkoa huo kiuchumi, kulia ni Mbunge viti maalumu mkoa wa Songwe Juliana Shonzana.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve (wa pili kulia) akikabidhi kiasi cha kiasi cha pesa shilingi laki Sita (600000) kwa akina mama wa UWT kata ya Ukumbi katika ziara aliyoifanya mwishoni mwa wiki ikiwa ni moja ya ahadi zake za kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuwainua akina mama wa mkoa huo kiuchumi, kulia ni Mbunge viti maalumu mkoa wa Songwe Juliana Shonzana.
Mbunge viti maalumu mkoa wa Songwe Juliana Shonzana akipokea zawadi kutoka kwa akinamama wa UWT kata ya Ukumbi katika ziara iliyofanywa na Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve mwishoni mwa wiki hii.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve wakifurahia jambo na wanawake wa UWT Kata ya Ukumbi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad