HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 20, 2017

JESHI LA POLISI LAWATAKA WAFANYA BIASHARA KUOMBA ULINZI WANAPOKUWA WAKISAFIRISHA FEDHA.


 Msemaji wa Jeshi la polisi,Advera Bulimba akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya  wananchi kuwa makini pindi wanapofanya biashara kwa njia ya mitandao kwa sababu wananchi wengi wamekuwa wakiibiwa kwa kutokuchukua tahadhari za kutosha,leo jijini Dar es Salaam.

Na Emmanuel Masaka, Globu Jamii.
JESHI la polisi limewataka wafanya biashara kuhakikisha kuwa  wanaomba ulinzi kutoka jeshi la polisi au makampuni binafsi ya ulinzi yanayo husika na kusafirisha fedha ilikupunguza matukio ya kuvamiwa na kuibiwa fedha wanapokuwa wakisafirisha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo hii Jijini Dar es salaam Msemaji wa Jeshi la polisi Advera Bulimba   amesema uchunguzi wa Jeshi la polisi umebaini kuwa uhalifu huo umekuwa ukisababishwa na wafanya biashara husika kutokuwa na usiri pamoja na kutokuomba ulinzi kutoka Jeshi la polisi au makampuni binafsi ya ulinzi yanayoshughulika na kusafirisha fedha.

‘’Jeshi la polisi nchini  linatoa wito kwa wafanya biashara kuhakikisha kuwa wanaomba ulinzi kutoka jeshi la polisi aumakampuni binafsi ya ulinzi yanayoshughulika na kusafirisha fedha pia  wasafirishaji wa fedha kuwa na usiri katika michakato yote inayohusiana   na usafirishaji wa fedha ilikuweza kupunguza matukio ya hayo’’ amesema Advera. 

Aidha Msemaji huyo amesisisitiza kuwa  wananchi kuwa makini pindi wanapofanya biashara kwa njia ya mitandao kwa sababu wananchi wengi wamekuwa wakiibiwa kwa kutokuchukua tahadhari za kutosha kabla  ya kutuma fedha.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji wa Jeshi la polisi,Advera Bulimba leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad