HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 29, 2017

Jaji nchini Marekani azuia amri ya Trump ya kuwarejesha makwao raia wa kigeni wenye viza

 Jaji wa Mahakama ya Federali nchini Marekani ametoa hukumu ya dharura ya kuzuia kurejeshwa makwao wasafiri wenye viza za kuingia nchini humo wanaozuiliwa kwenye viwanja vya ndege ili kutekeleza amri ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo.

Jaji Ann Donnelly amewakataza maafisa wa mipaka kumwondoa mtu yeyote aliyewasili nchini Marekani akiwa na viza yenye itibari au kibali cha ukimbizi kutoka moja ya nchi saba za Kiislamu zilizoathiriwa na amri ya Trump.

Amri hiyo iliyosainiwa na rais wa Marekani inapiga marufuku kuingia nchini humo katika kipindi cha siku 90 raia kutoka Iran, Iraq, Syria, Yemen, Sudan, Libya na Somalia; inawazuia pia wakimbizi kutoka Syria kuingia Marekani kwa muda usiojulikana na vilevile imesimamisha utoaji vibali vyote vya kuingia wakimbizi nchini humo kwa muda wa siku 120.

Japokuwa uamuzi uliotolewa na Jaji wa Mahakama ya Federali ya Marekani ambaye alichaguliwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Barack Obama ni kizuizi cha muda kwa amri iliyotolewa na Trump, lakini inaonekana kama pigo kubwa kwa hatua ya serikali mpya ya Washington dhidi ya wahamiaji.

Hayo yamejiri katika kipindi cha chini ya siku moja tangu raia wawili wa Iraq wawekwe kizuizini mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa John F Kennedy mjini New York jana asubuhi. Umoja wa Kutetea Uhuru wa Kiraia Marekani (ACLU) ulifungua kesi jana hiyohiyo kwa niaba ya Wairaqi hao huku ikikadiriwa kuwa watu kati ya 100 hadi 200 watakuwa wamekumbwa na mkasa huo wa kuzuiliwa kwenye viwanja vya ndege au visimamo vya muda kote nchini humo…

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad