Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo (wa tatu kushoto) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda Mhandisi Irene Muloni (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Hafla ya Uzinduzi wa Usanifu wa Awali wa michoro ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda Hadi Bandari ya Tanga Tanzania mjini Kampala Uganda.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha Wageni katika Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda baada ya kuhudhuria Hafla ya Uzinduzi wa Usanifu wa Awali wa Michoro ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania. Wengine wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Marwa Petro.
Waziri
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo tarehe 9/1/2017 aliongoza Ujumbe
wa Tanzania jijini Kampala nchini Uganda katika hafla ya Uzinduzi wa
Usanifu wa Awali (Front End Engineering Design -FEED) wa mradi wa Bomba la
kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga,
Tanzania.
Uzinduzi
huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini ya
Uganda na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri wa nchi
zote mbili za Uganda na Tanzania, Makatibu Wakuu wa nchi zote mbili,
Wakurugenzi wa mashirika ya mafuta na gesi, Kampuni zilizogundua mafuta nchini
Uganda za Total (Ufaransa), CNOOC (China), TULLOW (Uingereza), Kampuni ya Mafuta
ya Uganda National Oil Co. (UNOC), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
na wawakilishi wa vyombo vya habari.
Wakati
wa uzinduzi huo ilielezwa kuwa, FEED ni moja ya hatua muhimu katika
kuhakikisha mradi huo unatekelezwa katika viwango vinavyozingatia usalama wa
kimazingira na ustawi wa jamii.
Vilevile, ilielezwa
kuwa, hatua hiyo itajumuisha pia upatikanaji wa njia ya gharama nafuu ya
kupitisha bomba la mafuta ambapo pia Wataalamu wa taaluma mbalimbali watahusika
katika kuhakikisha mradi huo unafuata viwango na ubora wa kimataifa.
Pia
, imeelezwa kuwa bomba hilo litakuwa la kwanza kwa urefu duniani kuwa
bomba linalopashwa joto muda wote kutokana na asili ya mafuta yanayosafirishwa.
Mradi
huo mkubwa utatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali za Uganda na Tanzania na
pia utahusisha kampuni za TOTAL, CNOOC na TULLOW.
No comments:
Post a Comment