HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 17, 2017

ASILIMIA 90 SASA MKWASA KURUDI YANGA


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KLABU ya Yanga imeonesha nia ya kumrudisha aliyewahi  kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Charles Boniface Mkwasa kwenye klabu hiyo kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.

Kwa habari za ndani ya Yanga zinasema kuwa Mkwasa atakuja kuongeza nguvu kwa timu yao kwani kwa sasa wanahitaji mtu mwenye uelewa mkubwa wa soka la Tanzania na kuonesha lengo la kumchukua baada ya kumaliza kandarasi yake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).

Mkwasa anasadikiwa kupewa cheo kikubwa zaidi kitakachokuwa kinampa nafasi ya kusimamia timu zote ikiwemo za vijana na kutafuta vipaji nchi nzima na kuvikuza.

Taarifa rasmi ya kuja kwa Mkwasa inaweza ikatolewa hivi karibuni huku uwepo wa Juma Mwambusi kwenye benchi la wanajangwani hilo likiwa halijaweka wazi kama wataendelea nae au kumkacha.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad