HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 11, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA: USIKU WA TUZO YA EATV, WACHEKI HAPA WALIOTISHA ZAIDI KATIKA USIKU HUO

Desemba 10, 2016 ndio ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi hasa Wasanii wa Muziki na Filamu hapa nchini, kwani ndio ilikuwa na Usiku wa Tuzo zilizoandaliwa na Kituo mikubwa cha televisheni hapa nchini cha East African na tuzo hizo kubeba jina la EATVAWARDS 2016. Katika usiku huo, Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Alikiba ndie aliyeng'ara zaidi kuliko wengine, kwani alinyakulia Tuzo tatu muhimu katika vipengele vya Wimbo bora wa Mwaka, Msanii Bora wa Kiume na Video bora ya mwaka. kwa Upande wa Filamu Msanii Salim Ahmed maarufu kama 'Gabo Zigamba' akiondoka na tuzo mbili ambazo ni Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume na Filamu bora. Tuzo ya Mwanamuziki bora wa kike ilikwenda kwa mwanadada Lady Jay Dee, Tuzo ya Kundi Bora la Mwaka ilikwenda Navy Kenzo, Tuzo ya Msanii chipukizi ilikwenda kwa mzee wa "Hainaga Ushemeji", ManFongo, Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kike ilichukuliwa na Msanii Chuchu Hans. Tuzo ya Heshima ilichukuliwa na Mkongwe Dj Bonny Love kufuatia mchango wake mkubwa katika tasnia ya Muziki wa Kizazi kipya, kiukweli kabisa tuzo hii imepelekwa sehemu husika kabisa kwani mchango wa Dj Bonny Love katika muziki wa Tanzania ni Mkubwa sana.

ENDELEA KUANGALIA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA HAPO CHINI.




































































































No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad