HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 13, 2016

"KISS ME" YA ISHA MASHAUZI KUACHIWA DESEMBA HII

Na  Humphrey Shao

Mwanamuziki wa muziki wa taarabu hapa nchini Aisha Ramadhani (Isha Mashauzi) anataraji kuachia kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Kiss Me.

Akizungumza na Globu ya Jamii Mashauzi amesema kuwa amekuwa kimya kwa kipindi kirefu hivyo kibao hicho kitaweza kuwarudisha mashabiki wake katika mstari.

“hii ni zawadi ya kufunga na kufungua mwaka kwa mashabiki wangu hivyo wajue kuwa nyimbo hiyo ambayo ipo katika viwango vya hali ya juu ambayo imefanywa katika studio za Sophia  zilizopo kinondoni” amesema Mashauzi

Ameongeza kuwa waliniona kuwa nimekuwa kimya katika taarabu sasa nimerudi tena na hichi kibao ambacho watafurahi wenyewe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad