HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 17, 2016

Bondia Francis Cheka kuzipiga leo na Singh huko India

 Ni Mjini New Delhi bendera ya Tanzania kwa mara nyingine katika michezo inapeperushwa na  Bondia  Francis Cheka ambaye anaingia ulingoni dhidi ya mpiganaji wa India Vijender Singh .

Kwa mujibu wa msomaji wetu Khadija, Deddah ambaye yuko nchini India pambano hilo linatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa.

Francis Cheka ambaye ni bingwa wa zamani  anapambana na  Singh ambaye anatetea taji lake la WBO Asia Pacific super middleweight.

Vijender ambaye alishinda taji hilo Julai mwaka huu kwa kumtandika bingwa wa zamani wa Ulaya Kerry Hope wa Australia mpaka sasa hajapoteza kitu ulingoni. 

Katika gemu hiyo ya raundi 10 Francis Cheka anatarajiwa kutumia uzoefu wake mkubwa kumtandika bingwa huyo na kumpokonya mkanda wake.
Wakati wa  upimaji uzito jana Francis alisema kwamba atazungumza ulingoni wakati Vijender akisema kwamba mkanda hauendi kokote utabaki nchini India.

Cheka mwenye umri wa miaka 34 ni veterani akiwa amepigana mara 43 na kushinda mara 32 zikiwamo TK 17.
Mpambano wa Cheka na  Singh utatanguliwa na mapambano mengine matano ya kirafiki ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad