HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 18, 2016

ALIKIBA AWA NYOTA WA MCHEZO, AMFUNIKA OKWI KWENYE MECHI YA HISANI NCHINI UGANDA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo fleva'  Alli Saleh Kiba "Ali Kiba" amecheza mechi ya kirafiki nchini  Uganda na kufanikiwa kupata tuzo ya mchezaji bora  'The Celebrity Player Award'  wa mechi hiyo iliyomshirikisha pia Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga Emanuel Okwi anayekipiga nchini Denmark.

"A celebrity For Charity Match" kama inavyojulikana, kwa mwaka huu  taasisi ya Dorah Mwima Foundation  ilimualika Ali Kiba kushiriki nao pamoja na kucheza mchezo huo wa kirafiki  ikiwa na malengo ya kuchangia kwa hisani katika mfuko wa akina mama wajawazito kuweza kujifungua salama.

Mchezo huo uliochezwa leo kwenye Viwanja vya Kabira Country Club umeambatana na burudani ya muziki kutoka kwa msanii huyo kutoka Tanzania huku ikiwa ni mara ya tatu kufanyika kwa tamasha hili linalojulikana kama Launching of the Mama Port Project

 Msanii Ali kiba akiwa na watu mashuhuri wengine walioshioriki katika mechi hiyo ya mfuko wakuchangia  wakina mama wajawazito wajifungue salama wakiwa na kikombe chao baada ya kushinda mchezo huo wa hisani, wa pili ktoka kulia Dora Mwina Mwanzilishi wa Taasisi ya Dora Mwina Foundation.

Mwanzilishi wa Taasisi ya Dora Mwina Foundation, Dora Mwina akisalimiana na msanii Ali kiba kabla ya mechi kuanza.
Msanii Ali kiba akiwa na kikombe chake alichokabidhiwa baada ya mechi kumalizika  akizawadia kama nyota wa mechi hiyo  akiisaidia timu yake kushinda kwa kufunga goli moja kati ya manne.
Msanii Ali kiba akiwa na shambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga Emanuel Okwi anayekipiga nchini Denmark.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad