Mtaa Kwa Mtaa Blog

ZOEZI LA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA BURE KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO LIMEENDELEA KATIKA MIKOA YA IRINGA NA NJOMBE

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imebuni na kuanza kutekeleza mpango wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa bure kwa watoto wenye umri chini ya Miaka mitano.
Akizungumza na wanahabari Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu RITA Emmy Hudson amesema kuwa mpango huo umebuniwa ili kuleta suluhisho la changamoto iliyokuwa ikisababisha watoto kushindwa kusajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa kwa wakati.
Aidha amesema kuwa mpango huo ambao ulianza katika Mikoa ya Mwanza, Mbeya na Songwe hivi karibuni ulizinduliwa katika mikoa ya Iringa na Njombe hivyo basi ni mpango endelevu na wa kudumu.
Emmy ameongeza kuwa utekelezaji huo umefanikiwa kwa mikoa hiyo ambapo Njombe imepanda kutoka 8.5% ya watoto walisajiliwa hadi kufikia 98%.
 Kaimu Afisa Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa bure kwa watoto wenye umri chini ya Miaka mitano leo jijini Dar es Salaam kulia ni Meneja Usajili (RITA) Angela Anatory na kushoto ni Mkurugenzi wa Tehama(RITA) Cuthbert Simalenga
 Meneja Usajili (RITA) Angela Anatory akifafanua jambo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu Afisa Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya  jamii
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget