Mtaa Kwa Mtaa Blog

YANGA YAMUANGUSHIA JUMBA BOVU MWAMUZI WA MECHI YAO DHIDI YA MBEYA CITY

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BAADA ya kushindwa kufurukuta mbele ya Mbeya City benchi la ufundi la Yanga limemshushia lawama mwamuzi wa mchezo huo Mrope Rajab kuwa aliwaumiza katika kufanya maamuzi yake kwenye mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kufungwa 2-1.

Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema kuwa ni kweli wachezaji wake waliteleza lakini refa wa mchezo huo amewaumiza kwa maamuzi yake yake aliyoyafanya kwa kuruhusu wachezaji wa Mbeya City kupiga mpira wa adhabu kabla wachezaji hawajamaliza kujipanga.

"mwamuzi ametuumiza kwa kufanya maamuzi ambayo yaliwatoa  mchezoni wachezaji wake na kilipelekea kusababisha vurugu kwa kutoa maamuzi yanayotatanisha ,"amesema Mwambusi.

Mwambusi amesema tumeteleza na refa ametuumiza kwani aliombwa apime hatua ili kuweza pigo la adhabu kupigwa na  akakubali lakini wachezaji wa Mbeya City wakaanzisha mpira wakati golikipa bado akiwa anapanga wachezaji.

 Kutokana na tukio hilo ilibidi benchi la ufundi wawatulize wachezaji ambapo tayari wakatoka mchezoni na morali na kwanii goli la kwanza hawakulikataa iweje la pili waumie sana.


Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget