Mtaa Kwa Mtaa Blog

YAH TMK Taarab kutambulisha nyimbo mbili alhamis

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BENDI ya muziki wa taarabu  'Yah TMK Modern Taarab' inatarajia kufanya utambulisho wa nyimbo zake mbili za mwanzo, utakaofanyika Alhamis ya Novemba 10 mwaka huu.

Akizungumzia kuelekea uzinduzi huo Mkurugenzi wa bendi hiyo Said Fella, amesema kuwa  utambulisho huo maalum utaanza katika vyombo vya habari kwa kuanza kupiga nyimbo hizo katika vituo vya hapa nchini.

Fella amesema nyimbo hizo mbili ambazo tayari zimesharekodiwa  zimeimbwa na wanamuziki mahiri ambao ni Mwanahawa Ali aliyeimba wimbo wa "Sina Pupa" na Aisha Vuvuzela aliyeimba wimbo wa 'Kibaya kina Wenyewe' .

Bendi hiyo inaundwa na wanamuziki mahiri wa muziki huo , Mussa Mauji, Mussa Mipango, Omar Tego, Fatuma Nyoro, Mauwa Tego, Babu Kijiko na wengine waliopo kwenye bendi hiyo wanatoka kwenye kituo cha Mkubwa na wanawe ni pamoja na Mwanadada Jeza,Hassan Dogo na Ibrahim.

Fella amesema kuwa hata hivyo wataendelea kurekodi nyimbo nyingine na kuzitambulisha kama mwendelezo mpaka kufika uzinduzi wa albamu na bendi yao hiyo.

Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget