HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 21, 2016

WAZIRI POSSI ATEMBELEA VITUO NA SHULE ZA WATU WENYE ULEMAVU MIKOA YA MWANZA NA SIMIYU.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na baadhi ya Watendaji wa Serikali katika Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kutembelea vituo na shule za watu wenye Ulemavu tarehe 20 Novemba, 2016.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na baadhi ya watendaji wa Serikali (hawapo pichani) katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu alipofanya ziara ya kikazi.

Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano S. Mwera akizungumza na watendaji wa Kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Lamadi (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi Novemba 20, 2016 Mkoani Simiyu.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu)Mhe. Dkt. Abdallah Possi akipokea mafuta maalumu ya ngozi kwa watu wenye ualbino kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha kuhudumia watoto wenye Ualbino cha Lamadi Bi. Hellen Ntambulwa ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa ziara yake kituoni hapo. Novemba 20, 2016

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wenye ualbino wanaolelewa na Kituo cha Lamadi Wilayani Busega Mkoa wa Simiyu.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akimsikiliza Mwandishi wa habari wa ITV Bw. Berensi China wakati wa ziara yake Kituo cha kulelea watoto wenye Ualbino cha Lamadi Simiyu. 

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad