Mtaa Kwa Mtaa Blog

WAZAZI WAMESHAURIWA KUWALEA WATOTO WAO KATIKA MAADILI MEMA ILI TAIFA LIONDOKANE NA MATENDO MAOVU


Na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii 
Wazazi wameshauriwa kuwalea watoto wao katika maadili mema ili Taifa liondokane na matendo maovu. Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Naibu Mkuu wa Madrasatul Musbah iliyopo Mtaa wa Nzasa na Kigoma manispaa ya ilala, Sheikh Kassim Mzee.

Akizungumza katika Tamasha la wazi kati ya Madrasa na Wazazi iliyoandaliwa na Madrasa hiyo, Sheikh Mzee amesema ni vyema watoto wakaandaliwa katika maadili mema mapema kama ambavyo wao wanafanya katika madrasa yao kwa kuwafundisha mambo mbalimbali kwa lugha ya kiarabu kwa lengo la kumjua Mwenyezi Mungu kwakuzingatia yale aliyoamrisha na yale aliyoyakataza.

Tamasha hilo la siku ya wazi kati ya Madrasa na Wazazi Sheikh Mzee amefafanua kuwa wameamua kufanya tamasha hilo kwa lengo la kuwaonesha wazazi jinsi wanavyotakiwa kuwafundisha watoto wao (wanafunzi), ambapo wanafunzi hao wanaonesha kwa vitendo yale waliyokuwa wanajifunza darasani, nakudai kuwa huo ni mwanzo ila watajitahidi kufanya matamasha kama hayo kila mwaka, ili kuleta chachu kwa wazazi wengine kuona umuhimu wa kuwapa elimu watoto wao na kuwa watoto wema katika jamii.
 Naibu Mkuu wa Madrasatul Musbah iliyopo Mtaa wa Nzasa na Kigoma,Sheikh Kassim Mzee akizungumza na waandishi wa habari juu wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema ili Taifa liondokane na matendo maovu leo jijini Dar es Salaam.
  Wanafunzi wa madrasatul Musbah wakionyesha kwa vitendo namna ya kumuandaa maiti kabla ya kwenda kuzika leo Jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wazazi na wanafunzi wakiwa katika tamasha la wazi kati ya Wazazi na Madrasa leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget