Mtaa Kwa Mtaa Blog

VIJANA WA KITANZANIA KUPEWA ELIMU YA UJASIRIAMALI KUTOKA THUD YA NCHINI AFRIKA KUSINI


 Muanzilishi wa  The Hook Up Dinner (THUD)Selebogo Molefe (mwenye kofia) akiwa katika picha ya pamoja na vijana wengine kutoka Afrika Kusini na mwakilishi wa THUD Tanzania Baraka Mtavangu (wa kwanza kushoto) na Msimamizi wa ziara Uratibu na habari ,Matukio Chuma.
 Muanzilishi wa The Hook Up Dinner (THUD)Selebogo Molefe (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuhusiana na uzinduzi wa THUD nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika kesho. Kushoto ni Meneja uendeshaji wa THUD Tanzania Baraka Mtavangu.

 Msimamizi wa ziara uratibu na habari  Matukio Chuma akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio huo ambao utakuja kuwa na mafufaa kwa vijana hususani wajasiriamali wa hapa nchini.

                                  Na Zainab Naymka, Globu ya Jamii
THE Africa Entrepreneurship Compass (AEC) kutoka nchini Tanzania kwa kushirikiana na The Hook Up Dinner (THUD) kutoka Afrika Kusini wamedhamiria kutoa elimu wa vijana kuhusiana na ujasiriamli pamoja na kukutana nao kwa pamoja ili kufahamu changamoto wanazokutana nazo.

Ujio huo unakuwa ni kwa mara ya kwanza kuja hapa Tanzania na tayari wameshawasili nchini wakiwa viijana kumi na mbili kutoka Afrika Kusini na wanatarajia kufanya uzinduzi wa THUD nchini kesho huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage pamoja na Mkurugenzi wa makampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji.

THUD ni jumuiko kubwa la wajasiriamali kwa lengo la kuunganisha wajasiriamali wasiopungua milioni moja duniani hususani barani Afrika na  ilianzishwa mwaka 2012  Kijana Selebogo Molefe na mpaka sasa imeshajikita katika nchi kadhaa ambzo ni Afrika Kusini, Zimbabwe, Botswana, Lesotho, Kenya, Israel, Australia, Msumbiji, Hull City Uingereza, Zambia na Mauritius. 

AEC iko chini ya mtanzania Fay Nicholaus Shao imelenga zaidi kuwaunganisha wajasiriamali na kuunganisha nchi kulingana na mahitaji mara ya kwanza sasa Tanzania na  inatarajia kuwaunganisha wajasiriamali na fursa zilizopo kwenye uwekezaji Afrika na Dunia ikiwa inalenga na kutegemea kuwaleta pamoja wajasiriamali wasiopungua milioni moja.
siriamali wasiopungua milioni moja.

Safari hii isingewezekana kama si kwa ushirikiano wa hali ya juu na wa kipekee wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Naibu Balozi Mama Rosemary Chambe Jairo, Wizara ya Mambo ya Nje na idara ya Diaspora,msimamizi wa ziara Uratibu na Habari inayosimamiwa Matukio Chuma

Naye Meneja uendeshaji wa THUD Tanzania  Baraka Mtavangu amesema kuwa THUD  iko tayari na wamewasili  na uzinduzi rasmi utakuwa Novemba 18 mwaka huu na  wajasiriamali wote wanakaribishwa kwani hakuwatuwa na kiingilio chochote  pia anawshukuru sana  SAB South Africa Kickstart kwa kusaidia ujio huu nchini Tanzania.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget