
Akizungumza kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Kabete amesema kuwa lengo lake ni kuwa mmoja wa wawakilishi bora katika shindano hilo na kuitangaza vyema nchini pamoja na kurudi taji hilo na kwa kupitia kampuni ya Millen Magese Group chini ya Mkurugenzi wake ,Happiness 'Millen' Magese ameshukuru kwa kuingia nae mkataba ili aweze kushiriki michuano hiyo na kufanya Kazi nyingine za urembo.
"Mimi kama mwakilishi wa Tanzania nitahalikisha anafanya vizuri katika shindano hilo, ambalo nimepata nafasi ya kuwa mpeperusha bendera wa nchini yangu Tanzania " amesema. Kabete alikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ambaye alimshihi kwenda kujituma zaidi kwani wana imani na uwezo wake na pia ni moja ya warembo watakaowakilisha vyema nchi yetu na kurudi na taji hilo.
“Lengo la Serikali ni kuhakikisha washiriki wa shindano la Miss Tanzania wanapata fursa nyingine si tu akishapatikana mshinda wengine wanaachwa, hivyo tunaamini mrembo huyo anavigezo vyote na atakwenda kufanya vizuri,” amesema Nape.
Shindano hilo litafanyika nchini humo katika jimbo la Cross River, mji wa Calabar,ambapo Gavana wa jimbo hilo la Cross River Profesa Ben Ayade, atatoa zawadi ya gari na zaidi ya sh.million 52 ya Tanzania hiyo itakuwa kwa ushindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata zawadi ya Sh.milioni 32 na ushindi wa Tatu ni Sh.million 22.
Shindano hilo la Miss Afrika 2016 ambalo limebeba kauli
mbiu ya Kutunza, Kujali na Kuthamini Uchumi wenye kutoa kipaumbele kwa Mazingira kama nyenzo kwa ajili ya Maendeleo endelevu.
Julietha alichaguliwa katika shindano lililoendeshwa na kampuni ya Millen Magese (MMG), inayoshughulika na kusaka vipaji vya warembo pamoja na
Mmratibu wa MMG, Matukio Chuma, amesema kuwa wanamitindo kutoka kwenye shindano hilo wameweza kuendelea kufanya vizuri kupitia Swahili Fashion Week.
Taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli zake ndani na nje ya bara la Afrika, ikiwemo nchini Marekani, Millen Magese amekuwa Kinara, Balozi wa kuheshimika na aliye mfano ndani na nje ya Bara la Afrika. mwisho
No comments:
Post a Comment