HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 24, 2016

MBUNGE RUFIJI AWATAKA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUMUENZI HAYATI BABA WA TAIFA ILI KUJIEPUSHA NA MAPIGANO

NA VICTOR MASANGU,  RUFIJI
JAMII ya wakulima na wafugaji   Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani  wametakiwa kuachana  kabisa na vitendo vya vurugu na mapigano ya mara kwa mara na badala yake sasa wawe wazalendo na nchi yao kwa kumuhenzi hayati baba wa Taifa Mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere ili kuweza kurudisha hali ya amani na utulivu.

Hayo ameyasema wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kilimani kata ya Ngorongo katika mkutano wa adhara ambao ulifanyika   kufuatia kutokea kwa vurugu kubwa  zilizojitokeza  na  kuweza kusababisha vifo vya watu wawili.

Mchengerwa alisema kwamba  wakati wa uhai wa hayati  baba wa Taifa kulikuwepo na hali ya amani na utulivu katika maeneo yote, hivyo wananchi wa rufiji hususan kwa jamii ya  wakulima na wafugaji ambao ndio wamekuwa na migogoro ya muda mrefu wanapaswa kubadilika na kuwa na mtazamo chanya wa kupendana ili kuweza kudumisha mahusiano mazuri yaliyokuwepo katika kipindi cha miaka ya nyuma.

Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akifafanua jambo katika mkutano huo uLiofanyika katika kijiji cha Kilimani

 Baadhi ya wananchi hao wa kijiji cha Kiimani wakiwa katika mkutano huo kumsikiliza Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa

“Labda mimi kama  Mbunge wenu wa Jimbo la Rufiji nianze kw akusema kuwa ni lazima sasa tubadilike  kutokana na hali hii ya kuwepo kwa vurugu na mapigano ya mara kwa mara,na kikubw azaidi tufuate misingi mizuri ya kuependana na kushirikiana kwa hali na mali ambayo ameiacha hayati Baba wa Taifa kwa hivyo kwa hili naomba sana  tumuenzi Mwalimu Nyerere,”alisema Mchengerwa.

Alisema kuwa  ana imani endapo wananchi wake wa Rufiji wakizingatia maadili ambayo yalikuwa yakitolewa na Mwalimu Nyerere kutaweza kuleta mabadiliko makubwa katika suala zima la kimaendeleo ya kuondokana kabisa na hali ya kuwepo kwa mapigano ya mara kwa mara baina ya  wakulima na wafugaji.

“Hii hali ya kupigana wenyewe kwa wenywe na kusababisha vifo vya watu katika jimbo langu la Rufiji kwa kweli nataka imalizike kabisa, sipendi kuona wakulima na wafugaji wanafikia hatua ya kuwa maadui wakubwa wakati sisi sote ni wamoja na ni Watanzania kwa hiyo hapa kitu cha msingi kinachohitajika ni kuheshimiana na kulindana ili kuondokana na tatizo hili ila angekuwepo Mwalimu Julias Nyerere haya yote yasingeweza kutokea,”alisema Mchengerwa.

Katika hatua nyingine Mchengerwa amewataka wananchi wote wa Wilayani rufiji kuwa watulivu na wasifanye vurugu zozote kwani suala hilo la kuwepo kwa migogoro kwa sasa linafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo  na serikali ili kuweza  kuhakikisha  wananchi wote wanafanya kazi zao bila ya kuwepo kwa  uvunjifu wa amani.

Aidha amebainisha kuwa kwa sasa juhudi ambazo zimefanywa na halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ni kuhakikisha inawaondosha wafugaji wote ambao wameingia kinyume na sheria na taratibu na kwamba imeshawapa siku 30 ii wakatafute maeneo mengine ambayo tayari yalishatengwa maalumu kwa ajii ya shughuli za  ufugaji.

HIVI karibuni katika kijiji cha Kilimani kata ya Ngorongo kulizuka hali ya sintofahamu baada ya kutokea kwa mapigano kati ya wakulima na wafugaji na kusababisha vifo vya watu wawili, ambapo vurugu hizo zilitokana baada ya baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo yao mashambani na kufanya uharibifu mkubwa wa mazao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad