Baadhi ya Mashabiki wa Timu ya Mbeya city wakoma kumwanya wakishangilia ushindi wa gori 2,1 kwa kuibugiza timu ya Yanga leo katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
MABINGWA watetezi wa ligi kuu Vodacom Yanga wameshindwa kufurukuta mbele ya
Mbeya City baada ya kukubali kipigo cha goli 2,1 dhidi ya Mbeya City mchezo
uliochezwa katika uwanja wa CCM Sokoine jijini Mbeya.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi kwa timu ya Mbeya City kupata goli dakika ya
sita kupitia kwa Hassan Mwasapili ikiwa ni mpira wa adhabu uliopigwa nje ya 18 na
Kenny Ally kuaindikia goli la pili ikiwa nalo ni adhabu ambalo lilileta utata baada ya
mwamuzi kulikataa na kisha kulikubali.
Kutokana na hali hiyo wachezaji wa Yanga walianza kuliandama goli la Mbeya City na
katika dakika ya 45 ya kipindi cha Kwanza Donald Ngoma anaiandikia Yanga goli la
kufutia machozi ambalo lilidumu mpaka kipindi cha mwisho.
Na katika mchezo mwingine timu ya Simba imejihakikishia kuendelea kukaa kileleni
baada ya kuoata ushindi wa goli 10 dhidi ya Stand United baada ya mshambuliaji wao
Shiza Kichuya kuiandikia timu hiyo goli la uushindi kwa mkwaju wa penati.
baada ya matokeo hayo Simba imeendelea kujikita kileleni kwa alama 35 nyuma ya
alama 27 za mabingwa watetezi Yanga.
Mchezaji kutaka timu yaYanga Kelvin Yondani jezi Nambari 5 mgongoni akidhadhiana na muamuzi katika Mtanange wa Mbeya city na yanga Uwanjani Sokoine Jijini Mbeya..


Tuambieee Hilo ni Goriiii au sio Goriii....
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.
No comments:
Post a Comment