Mtaa Kwa Mtaa Blog

MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA ALIPOWAONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KATIKA MATEMBEZI YA HISANI YA AMREF

Makamu wa Rais wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan(katikati) akiongoza matembezi yaliyoandaliwa na Amref Health Africa kwa kushirikiana na Benki M yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusomesha wakunga nchini chini ya mpango wa S4UAM, matembezi yaliyokuwa na kauli mbiu “somesha wakunga kwa uzazi salama” yalianzia na kuishia katika viwanja vya Green, Oysterbay mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Waziri wa afya , Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu na Mkurugenzi mkuu mteule wa Benki M Bi. Jacqueline Woiso. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Amref Health Africa Dk. Florence Temu.
Makamu wa Rais wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiongoza mamia ya wananchi waliojitokeza katika matembezi yaliyoandaliwa na Amref Health Africa kwa kushirikiana na Benki M yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusomesha wakunga nchini chini ya mpango wa S4UAM, jumla ya Shilingi milioni 290 zilichangishwa katika matembezi hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “somesha wakunga kwa uzazi salama”.
Makamu wa raisi wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akishiriki katika mazoezi ya viungo baada ya kuongoza matembezi ya hisani ya “somesha wakunga kwa uzazi salama” mwishoni mwa wiki.
Makamu wa raisi wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha shukrani mkurugenzi mkuu mteule wa Benki M Bi. Jacqueline Woiso. Benki M ndio wadhamini wakuu wa matembezi hayo. Kushoto ni Waziri Wa Afya , Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu.
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget