Mtaa Kwa Mtaa Blog

HIVI NDIVYO MDAU NTIBASHIMA EDWARD ALIVYOLIKACHA KUNDI LA MAKAPERA


Bwana Harusi Ntibashima Edward ambae ni Mwajiriwa wa Kampuni ya Clouds Media Group inayomiliki Kituo cha Runinga cha Clouds pamoja na Clouds Fm, akimvisha Pete mke wake Bi Zitha Kannonyele, wakati wa Ibada ya ndoa yao iliyofungwa leo Katika Kanisa la Morovian lililoko Kimara Stop Over Jijini Dar es Salaam na Kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali walioalikwa kushuhudia tukio hilo muhimu kwa Wawili hao.

Bi Harusi Zitha Kannonyele akisoma mistari mitakatifu iliyoandikwa ndani ya Biblia, huku Bwana Harusi Ntibashima Edward, aliyevaa suti akisikiliza kwa makini maandiko hayo, tukio hilo limefanyika leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Ibada ya ndoa yao, ambayo imefanyika katika Kanisa la Morovian lililoko Kimara Stop Over.

Maharusi hao wawili wakisoma mistari mitakatifu iliyoandikwa ndani ya Biblia, wakati wa Ibada ya ndoa yao iliyofanyika leo katika Kanisa la Morovian lililoko Kimara Stop Over Jijini Dar es Salaam na Kuhudhuriwa na wageni mbalimbali walioalikwa Kushuhudia tukio hilo Muhimu kwa wanadoa hao.

Sophia Kessy na James Lyatuu ambao Wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi Ntibashima Edward , wakiwa wamepozi mbele ya kamera ya habari360.com, kwa ajili ya kupata picha ya Kumbukumbu.


Hapa wakiwa wamepozi na Bi Harusi Zitha Kannonyele kwa ajili ya Kupata Picha ya Kumbukumbu.
Maharusi Bwana Ntibashima Edward na Bi Zitha Kannonyele Wakijongea Kuelekea Kanisani ili Kutekeleza Ibada ya Ndoa yao, ambayo imefanyika leo Katika kanisa la Morovian lililoko eneo la Kimara Stop Over Jijini Dar es Salaam.
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget