Mtaa Kwa Mtaa Blog

UJENZI WA KITUO CHA POLISI KILUVYA WACHANGIWA NA NSSF.

 Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam  CP Simon Sirro akipokea hundi ya milioni 50 kutoka kwa  Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii  NSSF, Godius Kahyarara kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni.
 Mkurugenzi wa NSSF, Godius Kahyarara akizungumza na waandishi wa habari katika makabidhiano ya hundi ya milioni 50 kwa jeshi la Polisi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni. 
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, CP Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam baada ya kupokea hundi ya milioni 50 kutoka kwa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limechangia kiasi cha Milioni 50 kusaidia ujenzi wa kituo cha Polisi Kiluvya Gogoni ikiwa ni katika kukabiliana na changamoto ya kukua kwa miji kwenda sambamba na ongezeko la uhalifu.

Akizungumza wakati wa kutoa hundi ya milioni 50, Mkurugenzi wa NSSF, Godius Kahyarara amesema kuwa huu ni utaratibu wao katika kuisaidia jamii katika nyanja za elimu, Afya, Mazingira, Michezo na maeneo mengine yaliyoainishwa katika sera.

Kahyarara amesema kuwa kutokana na polisi kupanua wigo ili kufika katika matukio kwa haraka zaidi jeshi linahitaji kuongeza vituo maeneo mbalimbali na NSSF imeona vyema kushiriki katika suala zima la kuhifadhi na kulinda jamii na mali zao.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, CP Simon Sirro ameshukuru kwa hatua iliyochukuliwa na NSSF kwa kuweza kuwasaidia katika ujenzi wa kituo cha Kiluvya Gogoni kwani ulisimama kwa muda kutokana na ukosefu wa hela.

Akipokea hundi amewaomba mashirika mengine kujitokeza kusaidiana na polisi kuweza kuwasaidia kwenye ujenzi wa vituo ili kusogeza huduma ya haraka zaidi kwa wananchi pale matukio ya kiuhalifu yanapotokea.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget