Mtaa Kwa Mtaa Blog

MSAADA WA MADAWATI 100 YATOLEWA KATIKA SHULE YA MKWAKWANI NA TAASISI YA KARIMJEE JIVANJEE FOUNDATION.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella akipokea madawati 100 kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kulia) ikiwa ni msaada wa taasisi hiyo kwa shule ya Sekondari ya Mkwakwani iliyopo jijini Tanga jana. Anayetazama ni Meya wa Jiji la Tanga, Mustafa Selemani (kushoto).
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella akipokea madawati 100 kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kulia) ikiwa ni msaada wa taasisi hiyo kwa shule ya Sekondari ya Mkwakwani iliyopo jijini Tanga jana. Anayetazama ni Meya wa Jiji la Tanga, Mustafa Selemani (kushoto).

Taasisi ya Karimjee Jivanjee (KJF) imetoa msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 11 kwa shule ya Sekondari Mkwakwani mkoani Tanga. Msaada huu umetolewa ili kusaidia jitihada za serikali katika kupunguza uhaba wa madawati unaozikabili shule za msingi na za sekondari nchini. Akiongea katika hafla ya kukabidhi madawati hayo iliyofanyika kwenye shule ya Sekondari ya Mkwakwani katika manispaa ya Tanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee na Toyota Tanzania, Yusuf Karimjee alisema kwamba msaada huo ni sehemu ya mpango wa taasisi hiyo kusaidia sekta ya elimu nchini na uwekezaji katika miradi ya kijamii inayosaidia kuboresha maisha ya watu.

 “Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, KJF inachangia katika kujenga kizazi cha viongozi wajao, wakuu wa mashirika ya biashara, na wataalamu wataokuja kuchangia katika kuikuza nchi yetu kiuchumi,” alisema. Alisema kwamba KJF haijasubiri kuombwa na serikali msaada kutokana na kwamba tayari taasisi hiyo imekuwa ikisaidia sekta ya elimu kwa miaka mingi na ina azma ya kuendelea kufanya hivyo. 

Taasisi hiyo imekuwa siku zote ikiamini kwamba elimu ni msingi ambao utaijenga Tanzania imara, tasisisi imedhamiria kuisaidia sekta ya elimu kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa miongo kadhaa. Makabidhiano ya madawati hayo yaliambana na ahadi ya taasisi hiyo kuzisaidia na shule nyingine mkoani Tanga na kuendelea kuchangia maendeleo ya sekta hii kwa namna mbalimbali. Hafla ya kukabidhi madawati hayo ilishuhuiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, ambaye alisema kwamba madawati hayo yatasaidia kuboresha mazingira ya wanafunzi kusomea shuleni hapo na kuwaasa wadau wengine kujitokeza kujiunga na jitihada hizi kupunguza uhaba wa madawati katika mkoa huo.

 Mkuu huyo wa mkoa aliwashukuru KJF kwa kuupa kipaumbele mkoa wa Tanga na vilevile kusaidia elimu katika mikoa mingine nchini yenye kuhitaji msaada wa sekta binafsi. Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mkwakwani, Kavumo Mziray, aliishukuru KJF na kusema kwamba madawati hayo yatasadia kuboresha miundombinu na mazingira mazuri ya kujifunza yatakayosaidia jitihada za shule hiyo kufanya vizuri kitaaluma. Shule hiyo ya Sekondari ya Mkwakwani ilijengwa na familia ya Karimjee miaka 69 iliyopita ambapo imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na serikali katika kuendesha shule hiyo pamoja na shule nyingine nchini ikiwa ni utekelezaji wa azma ya kusaidia elimu katika mkoa wa Tanga na nchi nzima kwa ujumla.
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget