Mtaa Kwa Mtaa Blog

LILIANI KAMAZIMA MISS TANZANIA ANAEMALIZA MUDA WAKE, KAANDIKA HAYA KUELEKEA KUKABIDHI TAJI HILO LEO

Tanzania yangu,
Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniongoza, kunilinda na kunifikisha hii safari salama. 

Familia yangu ambayo haikunikatisha tamaa na kujitolea hata kwa kile kidogo ili tuu niweze kuwa na ule muonekano wa Miss Tanzania machoni mwa watu. 

Rafiki zangu wote mlionishabikia, kunipa msukumo zaidi na hata kunikosoa mlipohisi nakosea. 

Shabiki zangu wote mlioweza kunijenga hasa pale mlipokuwa mnanipa maoni yenu yaliyonipa changamoto na kunihamasisha kusonga mbele zaidi, mlinipigia kura mkijua sisimami mimi kama LILIAN KAMAZIMA bali kama TANZANIA pale nilipowakilisha taifa letu katika mashindano mbalimbali.

Viogozi, makampuni , mashirika mbalimbali, wanahabari , madesigner, wapiga picha, wafanyabiashara, walimu na madaktari wote walikuwa na msaada mkubwa sana kwangu kuhakikisha natimizi majukumu yangu.

Nawashukuru sana kwa miaka miwili ambayo sitoweza isahau katika maisha yangu. 

Ni heshima kubwa sana kuitwa MISS TANZANIA na hilo ndio jina langu mpaka sasa. Miss Tanzania imebadilisha mtazamo wa maisha yangu kabisa kwanzia kutembea hadi kazi nilizoweza kufanya. 

Miss Tanzania imenifungulia milango mingi sana kukutana na watu ambao hata sikuwahi kutegemea kuwajua, sehemu ambazo sikutegemea kufika, kazi nilizofanya na watu tofauti ili kuhakikisha naisaidia jamii yangu kwa namna moja au nyingine. 

Natazamia kuendeleza historia ya maisha yangu kwa kutumia nilichojifunza na yalionijenga mpaka kuwa LILIAN KAMAZIMA na kuendelea kuiwakilisha nchi yangu kwa kadiri niwezavo. 

Ahsante sana Tanzania,
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Africa.
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget