Mtaa Kwa Mtaa Blog

WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA NHIF ILI KUWA NA UHAKIKA WA MATIBU WAKATI WOTE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akinzungumza pindi alipotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuona namna wanavyotoa huduma wakati wa Mchezo wa hisani wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililoukumba Mkoa wa Kagera hivi karibuni, kwa kuzikutanisha Timu za Wabunge wapenzi wa Yanga na Wabunge wapenzi wa Simba, uliochezwa jana jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu ametoa wito kwa wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuwa na uhakika wa kupata matibu wakati wote. kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhi cheti kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga cha kutambua mchango wa NHIF katika tukio la tetemeko lililotokea mkoani Kagera.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Moses Nnauye akipima Afya kwenye Banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati alipowasili katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizari ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akipima Afya kwenye Banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati alipowasili Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget