Mtaa Kwa Mtaa Blog

WANAWAKE MKOA WA IRINGA WAASWA KUJIKITA KWENYE UJASILIAMALI.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Iringa, Rose Tweve amekutana na wakinamama wa wilaya ya Mafinga na kuwataka kuhakikisha wanajiingiza katika vikundi vya ujasiriamali, katika mkutano huo amewataka wakinamama hao kuacha kujibweteka na kusubiri kuletewa na wanaume zao bali wanatakiwa kujishughulisha ili kujiongezea kipato.

Mbali na hilo amewaasa wanawake na kuhakikisha wanakuwa macho na masikio kwenye jamii zao juu ya ubakaji Wa watoto na wawe wanatoa taarifa za watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Baada ya kumalizika kwa mkutano huo Mbunge huyo wa viti maalumu aliweza kuzungumza na wakinamama mbalimbali na kuweza kujua changamoto wanazokutana nazo na kuwataka wajitume kuweza kuepukana na utegemezi.
 Mbunge wa Viti Maalumu Iringa akibadilishana mawazo na moja ya akina mama wa Wilaya ya Mafinga wakati wa mkutano wake akiwataka kujiunga na vikundi vya ujasirimali.
                                      
Mbunge wa Viti Maalumu Rose Tweve akiwa anazungumza na wakinamama wa Wilaya ya Mafinga na kuwaasa kujiunga na vikundi vya Ujasiriamali pamoja na kuwapatia mbinu za kujiondoa kwenye utegemezi         


 Mbunge wa Viti Maalumu Iringa, Rose Tweve akiwa katika picha ya pamoja na wakina mama wa Wilaya Mafinga Mkoani  Iringa.    

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget