HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 21, 2016

SIMBA KUHAMIA UWANJA WA TAIFA, TFF KUKARABATI UWANJA WA UHURU.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.KUFUATIA timu  mbalimbali kulalamikia Uwanja wa Uhuru kutokana na nyasi zake na kuonekana kuisha na kusababaisha majeraha kwa wachezaji hasa wakati wakiteleza na kupata michubuko kwa wingi. Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF, limeamua kuhamishai mchezo wa Simba na Majimaji kupigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

Mbali na mchezo huo pia mechi ya African Lyon na Kagera Sugar utapigwa pia Uwanja wa Taifa mpaka pale marekebisho yatakapomalizika.Mabadiliko hayo yametokana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusitisha kwa muda kuutumia Uwanja wa Uhuru katika kipindi hiki ambacho limeanza kufanyia marekebisho sehemu ya uwanja huo ambayo ni ya nyasi bandia (artificial turf).

Hivyo, mechi ya Simba na Majimaji itafanyika Jumamosi, Septemba 24 wakati ile ya African Lyon na Kagera Sugar itachezwa Jumatatu, Septemba 26. Jumapili, Septemba 25 Uwanja Taifa utatumiwa kwa mechi ya timu za Wabunge za Simba na Yanga ili kuchangia waathirika wa janga la tetemeko lililotokea mkoani Kagera.

Mechi nyingine za Ligi Kuu ya Vodacom zitakazochezwa Jumamosi, Septemba 24 ni kati ya JKT Ruvu na Mbeya City (Mabatini), Ndanda na Azam (Nangwanda Sijaona), Tanzania Prisons na Mwadui (Sokoine), Mtibwa Sugar na Mbao (Manungu).

Jumapili kutakuwa na mechi kati ya Stand United na Yanga (Kambarage), na Ruvu Shooting na Toto Africans kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.

Kutokana na marekebisho yanayofanyika Uwanja wa Uhuru, mechi ya kundi ya A ya Ligi Daraja la Kwanza kati ya Ashanti United na Pamba iliyokuwa ichezwe Ijumaa, Septemba 23 kwenye uwanja huo sasa itafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad