Mtaa Kwa Mtaa Blog

Kiota cha maraha cha Posto Bella, Bunju jijini Dar

 Ukiwa ndani ya kiota hiki ni kama uko nje ya jiji la Dar es salaam. Yaani unasahau kabisa kama kuna kelele za watu na magari duniani. Ni sauti za ndege wazuri wa angani tuu ndio zinaburudisha masikio na macho … kelele na honi za boda boda na magari hazikuhusu kabisa!. 
Mandhari yake ni kama uko mkoa Fulani wenye baridi kali na mvua nyingi, umaridadi wa garden yake utakufanya ujione kama uko mkoa kama Mbeya ama Iringa vile! 

Posto Bella iko kwenye Miinuko ya Bunju A, 1.2km kutoka barabara ya lami ya Bagamoyo, ambayo inapokea upepo mwanana unaotoka Bahari ya Hindi (see breeze). Baridi inayosababishwa na upepo huo ndio inayokufanya ujisikie uko ndani ya Mbeya.

Unataka kupumzika au kuburudika na ndugu, jamaa na marafiki basi hapa ndio kiota mufaka. Faragha, utulivu na kiwango cha juu cha huduma kitakufanya ujute kuchelewa kuigundua sehemu hii.

Ni mahsusi kwa ajili ya watu wanaotafuta burudani yenye utulivu kama wapendanao, mikusanyiko ya kifamilia (family gatherings), Graduations, harusi za watu wachache, sherehe za kiofisi (corporate parties), birthdays, mitoko ya ki-group cha kazini, engagement parties, kitchen parties, bridal showers na mengineyo mengi. 

Ukumbi (garden yetu) ni bure, hatutozi hela yoyote. Pia ni mahali muafaka kwa mitoko ya familia kwa ajili ya lunch na dinner siku za weekend.

Tarehe 1-Oct-2016 tutakuwa na LIVE – Band na Lunch kwa ajii ya watu wote na hasa wanaokuwa na graduation ceremony pale NBAA siku hiyo. Lunch Buffet itatozwa Tsh 20,000 Pp. 

Bei zetu za vinywaji ni za kawaida sana. Kwa maelezo zaidi tupigie 0655123695 au email: postobellaresort@gmail.com
Picha zaidi tucheki kwenye Instagram: @posto_bella. Tafadhali tu-follow kwenye instagram uweze kupata habari za matukio mbali mbali kila mwezi.
Posto Bella is like Nowhere in Dar!


Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget