Mtaa Kwa Mtaa Blog

MSHINDI WA NZAGAMBA AONDOKA NA NG'OMBE WILAYANI MUSOMA

Mmoja wa wateja wa kinywaji cha Nzagamba mkoani Mara akiwa amefungwa kitambaa usoni ili kuvuruga kuponi za shindano la Nzagamba na baadaye kumchagua kuponi moja iliyopelekea Ndugu Majani Manyama aliibuka kuwa mshindi wa dume la Ng'ombe (Nzagamba) lililofanyika katika Eneo ya Bukima wilayani Musoma mkoa wa Mara. Kushoto ni Meneja mauzo na usambazaji wa kinywaji cha Nzagamba kanda ya ziwa, Peter Mwambenja na baadhi ya wateja wa eneo hilo.
Mshindi wa shindano la kunywa Nzagamba ushinde mkoa wa Mara, Majani Manyama (alieshika kofia mkononi) akikabidhiwa zawadi ya Dume la Nzagamba toka kwa mkuu wa kiwanda cha Nzagamba kanda ya ziwa, Helbert Ilembo mara baada kuibuka mshindi katika droo iliyocheshwa kwenye kitongoji cha Bukima wilayani Musoma mkoa wa Mara. kulia ni Meneja mauzo na usambazaji wa kinywaji cha Nzagamba kanda ya ziwa, Peter Mwambenja mwenye kofia nyekundu na katikati ni meneja mauzo ndugu James Makala.
Mmoja kati ya watumiajai wa Kinywaji cha Nzagamba mkoani Mara akifurahia kinywaji hicho wakati wa kufanyika kwa Droo ya kumtafuta mshindi wa shindano la Kunywa Nzagamba ushinde Dume la Ngombe, lililofanyika katika Eneo ya Bukima wilayani Musoma mkoa wa Mara.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget