Mtaa Kwa Mtaa Blog

MALOVEEE YANAPOGEUKA JANGA: Jamaa ang'atwa na kunyofolewa kipande cha ulimi na mwanamke aliyekuwa nae falagha

Mkazi wa Mandewa, Manispaa ya Singida, Said Mamba (24), amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida baada ya kung’atwa theluthi tatu ya ulimi wake na mwanamke waliyekuwa wakinyonyana ndimi.

Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, saa 3:30 usiku wa sikukuu ya Idd el Hajj.

Mamba, ambaye hawezi kuzungumza ametoa maelezo ya tukio hilo kwa njia ya maandishi.

Alisema siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari iliyopo eneo la Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake.

“Nilikubali kumsindikiza, tukiwa njiani aliniomba tufanye ZINAA . Nilipokataa alinilazimisha na baada ya kuona sitaki aliomba tuagane kwa kunyonyana ndimi, nilikubali ombi hilo,” alisema.

Mamba alisema wakati wakiendelea, mwanamke huyo alianza kumvua mkanda wa suruali lakini alimzuia ndipo alipomng’ata ulimi na kuondoka na kipande.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget