HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 17, 2016

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA VIZUIZI VYA BARABARANI (MIZANI)

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimsikiliza Msimamizi wa Kizuizi cha Vigwaza Mkoani Pwani Bw. Titus Michael wakati wa ziara yake kujionea hali halisi ya vituo hivyo kwaajili ya Maboresho ya mazingira ya biashara na Uwekezaji nchini. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiweka sahihi katika kitabu cha wageni wakati wa ziara yake katika Vizuizi vya barabarani (Mizani) na Mipakani kwa lengo la kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa mpango wa maboresho ya mazingira ya biashara na uwekezaji nchini Septemba 15, 2016.
Msimamizi wa Kituo cha Mamlaka ya Mapato TRA kilichopo Mkoani Pwani Bw. David Kisanga akitoa maelezo juu ya utendaji wa ofisi zao kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati alipotembelea ofisi hizo Mkoa wa Pwani.
Baadhi ya magari yakipima uzito wa mizigo katika Mizani ya Vigwaza mkoa wa Pwani, Septemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad